24.3 C
Dar es Salaam
Monday, September 16, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Bashe atangaza neema kilimo cha umwagiliaji Katavi

*Serikali yawekeza zaidi ya Sh Bilioni 55 Katavi

*Azindua ujenzi wa Maghala mawili na kuweka Jiwe la Msingi ujenzi wa Ukarabati wa Skimu ya Umwagiliaji

*Aishukuru Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa kutekeleza miradi zaidi ya 29 mkoani Katavi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe (Mb) ametangaza neema kwa wakulimo wa Mkoa wa Katavi na kusisitiza kuwa Serikali imedhamiria kuendelea kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji kwa zaidi ya Sh Bilioni 55 mkoani humo.

Waziri Bashe ametangaza neema hiyo katika kijiji cha Mwamkulu, wakati wa akizindua ujenzi wa maghala mawili na kuweka Jiwe la Msing la Ujenzi wa Ukarabati wa Skimu ya Umwagiliaji.

Ametumia fursa hiyo kusifu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) chini ya Uongozi wa Raymond Mndolwa kwa kutekeleza miradi zaidi ya 29 katika Mkoa wa Katavi.

Waziri Bashe amesema kuwa lengo la Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ni kuujengea uwezo mkoa wa Katavi na nchi nzima kwa ujumla, ili kuzalisha chakula cha kutosha cha kulisha ndani na nje ya nchi litafikiwa kutokana na uwekezaji huo mkubwa unaoendelea.

“Naomba kuwasilisha salamu za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye anaahidi kuja kushiriki katika uzinduzi wa miradi mingine ya Umwagiliaji katika Mkoa huu wa Katavi, ikiwemo Kata ya Mwamkulu kabla ya Uchaguzi Mkuu ujao,” amesema Waziri Bashe.

Waziri Bashe pia amewaasa wakulima wa Mwamkulu kuwa Mfuko wa Maendeleo ya Umwagiliaji ulianzishwa kwa ajili ya kuwezesha wakulima kuchangia kufanya marekebisho ya miundo mbinu na kuchangia kujenga maeneo mengine. Pia ametoa wito kwa wakulima kupata haki ya kumiliki maeneo yao kisheria kwa kuwa maeneo ambayo Serikali imewekeza lazima yalindwe.

Waziri bashe amebainisha kuwa Makubaliano ya Serikali ni kujenga miundombinu katika hekta 27,000 kwa wilaya zote mbili na kwamba imeanza na hekta 6000. “Malengo ya Serikali ni wakulima muweze kulima mara mbili hadi mara tatu kwa mwaka,” alisema Bashe.

Bashe amebainisha kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi katika miundombinu ya umwagiliaji na kuwa pamoja na uwekezaji huo, mashamba yanayowekewa miundombinu yataendelea kuwa mali ya wananchi.

“Kuna skimu zitafanyiwa utekelezaji ambazo ni skimu za Itenka 4500, kakese 3000, karema zaidi ya hekta 5,000.  Hekta zote 25000 zitangazwe mwaka huu,” amesema Waziri Bashe, huku akielekeza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kutangaza kwa wakati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles