Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Waumini wa Kanisa Halisi la Mungu Baba wakiongozwa na Mchungaji Kiongozi ‘Baba Halisi’ wamefanya ibada maalum ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu.
Ibada hiyo iliyofanya katika Uwanja wa Tegeta Nyuki jijini Dar es Salaam, yenye lengo la kumtakia heri na baraka Rais katika uongozi na utendaji wake katika kulionhoza Taifa la Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Aprili 14,2024 Kiongozi wa Kanisa hilo Baba halisi amesema kuwa viongozi mnamajukumu mengi pigeni kazi Kanisa la Baba halisi linawaombea utendaji wenu.
“Tunatambua Mchango wenu na Changamoto mnazopitia lakini tunafanya maombi kwaajilinya Rais Samia Suluhu na viongozi wake wote wafanye kazi kwa amani Taifa likiwa na utulivu.
Pia ameongoza “Tumeambatana na kufanya usafi katika maeneo ya Tegeta Nyuki yote ni katika kufanya usafi wa roho lazima kuwepo na usafi wa mwili na mazingira.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule amewapongeza kwa kufanya usafi katika maeneo ya Tegeta Nyuki na kusema ni Imani yake wakazi wa Tegeta wametakata na roho pia.
“Kwa kuwa mlianza na maombi kwa Rais Samia Suluhu na kuendelea na usafi ni matumaini yangu Tegeta wamekuwa safi na rohoni matendo mema ya Pasaka na Ramadhani yataendelea hatutasikia uhalifu wa aina yoyote ile.”amesema Mtambula.