30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Watumishi walipa faini Sh milioni 35 kwa uhujumu uchumi

Na DERICK MILTON-SIMIYU

WATUMISHI wanne wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu (Mauwasa) waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi katika mahakama ya wilaya hiyo, wamehukumiwa kulipa faini ya Sh milioni 35.7.

Kupitia kesi yao No.01 ya mwaka 2018, watumishi hao wakiongozwa na Meneja wa Mamlaka hiyo, walituhumiwa kuisababishia hasara serikali ya zaidi ya Sh milioni 30.7.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Taasisi ya Kuzuia na kupamba na rushwa (Takukuru) Mkoa wa Simiyu, iliwataka watumishi hao kuwa Lema Jeremia ambaye alikuwa Meneja wa Mamlaka hiyo.

Wengine ni Juma Mpenda ambaye alikuwa fundi mchundo, Edmond Mahungi Meneja Biashara pamoja na Sophen Patrick mfanyabishara, ambapo kesi yao ilikuwa chini ya Hakimu Mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Fredrick Lukuna.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa na Kamanda wa taasisi hiyo mkoa, Joshua Msuya, ilieleza kuwa watumishi hao walifikia hatua ya kulipa faini hiyo baada ya kufanyika kwa mazungumzo baina yao na mwendesha mashtaka.

Msuya alieleza kuwa baada ya mazungumzo hayo, watumishi hao walikiri makosa ambapo mbali na kutakiwa kulipa faini hiyo, Mahakama iliwahukumu kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya Sh 380,000 kila mmoja.

“Walilipa faini hiyo kuepuka kwenda jela, lakini katika makubaliano hayo ya kulipa hiyo hasara ambayo waliisababishia serikali, wanatakiwa kulipa Sh. Milioni 35,721,300 kulingana na makubaliano waliyowekeana,” alisema Msuya.

Katika hatua nyingine taasisi hiyo imeeleza kuwa imegundua kuwepo kwa dosari katika mifumo ya ukusanyaji wa kodi ya huduma (service levy) katika halmashuari za Wilaya ya Itilima, Maswa, Meatu, pamoja na Bariadi.

Katika uchunguzi wake Takukuru ilisema kuwa imebaini katika mifumo hiyo kuna udhaifu wa mifumo ya utambuzi wa walipa kodi ya huduma, pamoja na baadhi ya maofisa wa ukusanyaji wa kodi kuchukua fedha taslimu kwa walipa kodi (wananchi) bila ya kutoa risiti.

Aidha dosari nyingine ni walipa kodi walio wengi hawana elimu juu ya kodi wanazopaswa kulipa, pamoja na baadhi ya walipa kodi kukwepa kulipa kodi kutokana na halmashuari kushindwa kufuatilia ikiwa pamoja na kutochukuliwa hatua zozote za kisheria kwa wale wanaoshindwa kulipa.

Kutokana na hali hiyo Kamanda huyo wa Takukuru kwenye taarifa yake hiyo alisema kuwa wamepanga kufanya mkutano na wadau wa kodi mkoa, ili kujadili matokeo ya uchunguzi huo ambao wameufanya ikiwa pamoja na kuweka mikakati ya kukomesha hali hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles