23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mhandisi kortini kwa utakatishaji fedha

NA KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

MHANDISI Baraka Mtunga (43) na mwenzake amefikishwa mahakamani akituhumiwa kwa mashtaka sita ikiwemo kuongoza genge la uhalifu katika Hifadhi ya Saadani na kutakatisha zaidi ya Sh milioni 267.

 Mshtakiwa Mtunga na Rajabu Katunda (42) walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Kassian Matembele na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon akisaidiana na Jakline Nyantori.

Washtakiwa wanadaiwa kati ya Desemba 13 mwaka 2019 hadi Septemba 28 mwaka huu, katika Hifadhi ya Taifa ya Saadani katika jijiji cha Kanjoo, Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani, kwa pamoja kwa lengo la kupata faida, waliongoza genge la uhalifu.

Katika shtaka la pili, wanadaiwa kuwa, katika tarehe na maeneo hayo, walisimika na kuvitumia vifaa vya kielektroniki bila ya kuwa na leseni kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TCRA). 

Shtaka la tatu, wanadaiwa kuvitumia vifaa hivyo vya kielektroniki kwa ajili ya kusambaza mtandao wa internent yaani wife bila ya leseni kutoka mamlaka husika. 

Katika shtaka la nne, washtakiwa hao wanadaiwa kwamba wakiwa na nia ya kukwepa malipo halali ya kodi, walisambaza huduma hiyo ya internet. 

Inadaiwa katika shtaka la tano kuwa, kati ya Desemba 13 mwaka 2019 hadi Septemba 28 mwaka huu, katika Hifadhi ya Taifa ya Saadani katika jijiji cha Kanjoo, Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani na maeneo mbali ya jiji la Dar es Salaam,  waliisababishia TCRA hasara ya sh 267,656,794.30.

Shtaka la sita la utakatishaji fedha ambapo ilidaiwa kwamba, katika tarehe na maeneo hayo, washitakatiwa hao walijihusisha n amiamala mbalimbali ya Sh 267,656,794.30 huku wakijua fedha hizo ni zao la makosa tangulizi likiwemo la kuendesha genge la huhalifu kwa lengo la kujipatia faida.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, washtakiwa hawakutakiwa kujibu,.mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi. 

Wankyo alidai upelelezi wa kesi haujakamlika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa ambapo ilipangwa Oktoba 27 mwaka huu. Washtakiwa wako rumande.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles