25.2 C
Dar es Salaam
Saturday, September 21, 2024

Contact us: [email protected]

UTAFITI: WANAWAKE WANA MCHANGO MKUBWA UKUAJI WA UCHUMI

|Bethsheba Wambura, Dar es Salaam



Kituo Cha Haki za Binadam (LHRC), kimefanya utafiti ambao umebainisha kuwa wanawake wana mchango katika ukuaji wa uchumi hasa kupitia katika sekta isiyo rasmi na sekta binafsi.

Kwa mujibu wa utafiti huo, wanawake wamekuwa wakimiliki zaidi ya asilimia 50 ya biashara ndogo na kati (SME) licha ya changamoto kadhaa wanazopitia.

Hayo yamebainishwa leo Alhamisi Agosti 16, katika uzinduzi wa muhtasari wa Ripoti ya Haki za Binadamu na Biashara ya mwaka 2017 na Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga.

Akisoma ripoti ya utafiti huo, Henga amesema unyanysaji wa kijinsia, ikiwamo wa kingono unaofanywa na baadhi ya maofisa kwenye sekta ya biashara ni changamoto kwa wanawake.

“Wanawake wanapitia changamoto nyingi katika sekta ya biashara ikiwamo ya kunyimwa haki ya kumiliki mali, hivyo kukosa dhamana ya mikopo na kuna uelewa mdogo kuhusu masuala ya sheria na haki za wanawake katika maeneo mengi ya kazi.

“Aidha pia wanawake kutokuwa na mtaji wa kutosha wa kuanzisha biashara, sheria na kanuni kulenga zaidi makampuni makubwa na kusahau wafanyabiashara wadogo na wa kati  na kiwango kidogo cha elimu rasmi ya ujasriliamali, hizi ni changamoto zinazowakawamisha wanawake katika sekta ya biashara,” amesema.

Aidha Henga amesema kwa upande wa sekta ya viwanda, utafiti wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kuhusu wafanyakazi wa mwaka 2014 unaonesha kwamba wanawake walioajiriwa katika sekta ndogo za sekta hiyo ni 9,887 huku wanaume wakiwa 10,144.

Amesema wanawake sasa wanaajiriwa kufanya kazi ambazo hapo mwanzo zilionekana ni za kiume ikiwemo katika sekta ya usafirishaji madini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles