33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi wajisaidia vichakani

Na Gurian Adolf – Sumbawanga


WANAFUNZI wapatao 965 wa Shule ya Msingi Kalepula   katika Kijiji cha Kalepula wilayani Kalambo,   wapo hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na kujisaidia vichakani.

Hali hiyo inatokana na shule hiyo kutokuwa na  vyoo kwa   miezi sita baada ya vilivyokuwapo kubomoka.

Kwa sababu hiyo wanafunzi wamekuwa  wakijisaidia vichakani .

Mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo, Gerad Isack alisema kutokana na kubomoka vyoo shuleni hapo, wamekuwa katika wakati mgumu hivyo wanalazimika kwenda kwenye nyumba za jirani na shule kuomba kujisitiri.

Hata hivyo,  alisema wengi wao wamekuwa wakishindwa kuvumilia na kujikuta wakikimbilia vichakani  kujisaidia jambo ambalo ni hatari kwa afya zao.

Mwandishi   alimtafuta Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Gido Mtafya ambaye alikiri   shule yake kukabiliwa na changamoto hiyo ya ukosefu wa vyoo kwa wanafunzi.

Alisema kupitia kamati ya shule wamekwisha kulijadili suala hilo ikiwamo kukubaliana kuwaita wazazi   na kutoa taarifa kwa mkurugenzi kwa hatua zaidi.

Akizungumza kwenye sherehe za mahafali ya kuhitimu wanafunzi wa darasa la saba shuleni hapo, Katibu  wa Chama Cha Walimu  Tanzania (CWT) Wilaya ya Kalambo, Peter Simwanza, alitoa msaada wa mifuko 10 ya saruji na kuahidi bati bandari moja ikiwa ni kuhamasisha ujenzi wa matundu ya vyoo vya shule hiyo.

Pia alisisitiza kuna umuhimu wa wazazi kuendelea kuchangia michango shuleni hapo kukabiliana na changamoto badala ya kuisubiri serikali pekee.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles