29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yatakiwa kuwatumia wanaomaliza mgambo kwenye ulinzi

Susan Uhinga, Tanga



Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa, ameiomba Ofisi ya Mshauri wa Jeshi la Akiba wilayani hapa kuwasaidia vijana wanaopata mafunzo ya mgambo kujiunga ili waweze kufungua chombo cha pamoja kama vile kampuni.

Mwilapwa ameyasema hayo jana wakati akifungua rasmi mafunzo ya jeshi la akiba kwa vijana, ambao wameweka kambi katika Kata ya Chongoleani.

Amesema vijana hao watakapomaliza mafunzo yao wasaidiwe kufungua kampuni na kwamba kwa kufanya hivyo itawaidia kuweza kupata fursa katika maeneo ambayo wanahitaji huduma ya ulinzi.

“Naagiza taasisi mbalimbali wanaotaka huduma ya ulinzi wawatumie vijana hawa wanaomaliza mafunzo ya kijeshi na wengine,” amesema mkuu huyo wa Wilaya.

Kwa upande wao vijana hao wameiomba serikali kuwasaidia kuunda chombo cha pamoja mara baada ya kumaliza mafunzo ili waweze kufanya kazi za ulinzi kwenye tasisi mbalimbali.

“Tunashukuru Serikali kutupa fursa hii lakini tunaomba tutakapomaliza hapa tupate hata kazi za ulinzi kwenye huu mradi wa bomba la mafuta,” amesema Mwanahamisi Ramadhani ambaye ni mmoja wa vijana waliopo kwenye mafunzo hayo.

Vijana hao ambao wanatoka katika maeneo mbalimbali ya Kata ya Chongoleani, wapatao 162 watakuwa kwenye mafunzo hayo kwa muda wa miezi minne.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles