31.8 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Apandishwa kortini kwa kumchapa mtoto

ZAKIA NDULUTE (UoI) Na HAPPYNESS GRAYSON (UoI) – DAR ES SALAAM         |    


MKAZI wa Mikocheni A, Pyana Herbo (45), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni, Dar es Salaam kwa tuhuma za kumshambulia kwa mchapa   fimbo mtoto.

Karani wa Mahakama hiyo, Januari Kasekwa alidai  mbele ya Hakimu Marko Mochiwa kuwa Septemba 10 saa 4 asubuhi eneo la Mikocheni A, Wilaya ya Kinondoni, mtuhumiwa alimshambulia mtoto Christina Hebron kwa kumpiga na fimbo sehemu mbalimbali za mwili.

Mshtakiwa alikana  shtaka hilona alirudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana hadi Oktoba 5, mwaka huu, kesi itakapotajwa tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles