Na LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM
SERIKALI imepanga kuhamisha walimu wa ziada wa shule za sekondari kwenda kufundisha shule za msingi ili kukabiliana na upungufu wa walimu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhandisi Mussa Iyombe, hatua hiyo imefikiwa baada ya kufanya uhakiki wa idadi ya wanafunzi, mikondo na walimu katika shule za msingi na sekondari za Serikali.
“Uchambuzi unaonyesha kuwa upo upungufu mkubwa katika shule za msingi na sekondari kwa masomo ya sayansi na hisabati.
“Takwimu zinaonyesha kuwa kuna ziada ya walimu wa masomo ya sanaa kwenye shule za sekondari mikoa yote,” ilieleza taarifa hiyo.
Taarifa hiyo pia ilifafanua kuwa ili kuboresha ikama ya walimu, Serikali imeamua kuwahamisha walimu wa ziada wa masomo ya sanaa wa shule za sekondari kwenda kufundisha za msingi.
Aidha taarifa hiyo iliwaelekeza wakurugenzi wa mamlaka za Serikali za mitaa, kuwahamishia walimu hao katika shule za msingi zilizopo karibu na shule wanazofundisha.
“Kwa barua hii, unaombwa kuwaelekeza …………………………………..
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya MTANZANIA.