LONDON –UINGEREZA
WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Theresa May amesema neno pekee wanaloweza kuwaambia wakongwe walioshiriki operesheni ya kijeshi iliyoikomboa Ulaya kutoka mikononi mwa Wanazi wa Ujerumani, ni asante.
May alitoa katuli hiyo katika hafla ya kuadhimisha miaka 75 ya kumbukumbu ya operesheni hiyo ya kijeshi iliyoikomboa Ulaya, maarufu kama D-Day.
Maneno hayo ya May yalitoa mwangwi kwa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye naye aliwaambia wajeshi wa D-Day waliokusanyika kaskazini mwa Ufaransa kwamba tuna deni na “uhuru wetu”
Rais wa Marekani, Donald Trump baadae naye aliwaambia wakongwe wa Marekani kwamba wao ni fahari ya Taifa hilo.
Trump alitoa kauli hiyo wakati akiwa katika makaburi ya wapigania uhuru hao yaliyopo Omaha.
Mamia ya wakongwe hao walikusanyika huko Normandy kwa ajili ya maadhimisho yaliyojumuisha operesheni za anga, ardhi na maji.