28.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri wa kwanza anayeshiriki wazi mapenzi ya jinsia moja ateuliwa Israel

TEL AVIV- ISRAEL

MWANAUME wa kwanza  kutangaza wazi kuwa anashiriki mapenzi ya jinsia moja, Amir Ohana ameteuliwa kuwa waziri wa sheria na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.

Waziri huyo Ohana, kutoka chama cha Netanyahu cha Likud, ameteuliwa kuwa kaimu waziri wa sheria baada ya waziri aliyekuwepo kufukuzwa kazi.

Ohana, mwenye umri wa miaka 43, ni mfuasi sugu wa Netanyahu, na aliunga mkono hatua za kumlinda dhidi ya kushtakiwa.

Uteuzi wake unakuja siku kadhaa baada ya bunge kuvunjwa kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mpya.

Inaelezwa kuwa Ohana ametumia juhudi zake zote kuunga mkono muswada tata uliomuwezesha Netanyahu kuwa na kinga ya kutoshtakiwa.

Netanyahu alimfuta kazi waziri wa sheria aliyekuwepo madarakani, Ayelet Shaked, miezi mitatu iliyopita.

Chama cha Shake, ambacho kilikuwa sehemu ya serikali ya muungano wa Netanyahu, hakikupata viti vya kutosha kukiwezesha kurejea bungeni katika uchaguzi wa mwezi Mei.

Waisrael watafanya tena uchaguzi mwezi Septemba baada ya Netanyahu kushindwa kupata uungaji mkono wa kutosha kutoka kwa vyama kumuwezesha kuunda serikali ya mpito.

Ikitangaza uteuzi wake, ofisi ya waziri mkuu ilisema Ohana ambaye ana taaluma ya sheria ni mwenye uelewa mkubwa sana mfumo wa sheria.

Ohana ni mwanaharakati wa haki za wapenzi wa jinsia moja , ambaye anatetea ndoa za jinsia moja, jambo ambalo halitambuliki nchini Israeli isipokuwa kwa wale watakaoamua kufunga ndoa yao nje ya nchi . 

Mwaka jana alipinga muswada wa sheria uliopiga marufuku ubaguzi wa wapenzi wa jinsia moja kwa kuzingatia utambulisho.

Ingawa haki za wapenzi wa jinsia moja zinapingwa na jamii ya Wayahudi nchini Israeli, kwa ujumla taifa hilo limekuwa na mafanikio katika sheria inayowalinda wapenzi wa jinsia moja .

Ohana ni mmoja wa wabunge kadhaa waliotangaza wazi kuwa wanashiriki mapenzi ya jinsia moja na mwaka jana mji wa Israel uliopo karibu na Tel Aviv ulikuwa wa kwanza kuwa na Meya mpenzi wa jinsia moja anayetangaza wazi kuwa anashiriki mapenzi hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles