27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wakongwe, viongozi wa dunia waadhimisha D-Day

LONDON –UINGEREZA

WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Theresa May amesema neno pekee wanaloweza kuwaambia wakongwe  walioshiriki operesheni ya kijeshi iliyoikomboa Ulaya kutoka mikononi mwa Wanazi wa Ujerumani, ni asante.

May alitoa katuli hiyo katika hafla ya kuadhimisha miaka 75 ya kumbukumbu ya operesheni  hiyo ya kijeshi iliyoikomboa Ulaya, maarufu kama D-Day.

Maneno hayo ya May yalitoa mwangwi kwa  Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye naye  aliwaambia wajeshi wa D-Day waliokusanyika kaskazini mwa Ufaransa kwamba tuna deni na “uhuru wetu” 

Rais wa Marekani, Donald Trump baadae naye aliwaambia wakongwe wa Marekani kwamba wao ni fahari ya Taifa hilo.

Trump alitoa kauli hiyo wakati akiwa katika makaburi ya wapigania uhuru hao yaliyopo Omaha. 

Mamia ya wakongwe hao walikusanyika huko Normandy kwa ajili ya maadhimisho yaliyojumuisha operesheni za anga, ardhi  na maji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles