27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

WAKILI WA LISSU AKIMBILIA MAHAKAMA KUU

Na KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

MBUNGE wa Singida Magharibi, ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu ameendelea kusota rumande kwa zaidi ya saa 48 bila kufikishwa mahakamani.

Kutokana na hali hiyo, wakili wa mbunge huyo, Peter Kibatala ameamua kukimbilia Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuomba iingilie kati ili mteja wake afikishwe mahakamani au impatie dhamana.

Kibatala alisema hayo jana katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kumsubiri mteja wake kwa siku nzima bila mafanikio.

Wafuasi wa Chadema pia walishinda katika mahakama hiyo tangu saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni, wakisubiri kiongozi wao afikishwe mahakamani.

 “Tulitegemea leo (jana) aletwe mahakamani, mpaka muda huu saa kumi hajaletwa wala kupewa dhamana na polisi.

“Hakuna sababu zozote za msingi za kumnyima dhamana kwa sababu ni mtu anayefahamika, wakili na mbunge… sasa wanamnyima dhamana atakimbilia wapi?

“Wamemkamata bila kuwa na hati ya kumkamata na tulitegemea wao wanamtuhumu kwa kosa alilotenda Januari 4, mwaka huu, hivyo walikuwa na muda wa kutosha zaidi ya mwezi mmoja kupeleleza kesi na kuandaa hati ya mashtaka,” alidai Kibatala.

Wakati huo huo, Chadema kimelitaka Jeshi la Polisi kumwachia mwanasheria wao huyo baada ya kushindwa kumwandikia mashtaka yanayomkabili tangu walipomkamata Februari 6, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vicent Mashinji, alisema kitendo cha kumweka mahabusu muda wote bila ya kumpeleka mahakamani ni kinyume na sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles