27.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 7, 2023

Contact us: [email protected]

MFUMUKO WA BEI WAPANDA

Na MAULI MUYENJWA-DA ES SALAAM

MFUMUKO wa bei kwa mwezi Januari, mwaka huu, umeongezeka hadi kufikia asilimia 5.2 kutoka asilimia 5.0 Desemba, mwaka jana.

Hali hiyo inasababisha kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioisha, kuongezeka ikilinganishwa na kasi ya upandaji ilivyokuwa mwaka ulioishia Desemba 2016.

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Huduma za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo, alisema hayo jana, Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari.

Alisema farihisi za bei zimeongezeka hadi 105.92 Januari, mwaka huu kutoka 100.71 Januari, mwaka jana.

“Mfumuko wa bei ya bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa Januari, mwaka huu, umeongezeka hadi asilimia 7.6 kutoka asilimia 7.0 ilivyokuwa Desemba, mwaka jana,” alisema Kwesigabo.

Alisema mfumuko wa bei kwa mwezi Januari, mwaka huu kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.8.

“Mfumuko wa bei Januari, mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 0.8, ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 0.7 ilivyokuwa Desemba, mwaka jana na farihisi za bei zimeongezeka hadi 105.92 Januari, mwaka huu kutoka 105.04 Desemba, mwaka jana,” alisema Kwesigabo.

Alisema baadhi ya vyakula vilivyochangia kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja na mahindi kwa asilimia 16, unga wa mahindi asilimia 10, mchele asilimia 2.6, maharage asilimia 6.3, ndizi asilimia 5.8 na magimbi 5.3.

Alisema uwezo wa shilingi ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia Sh 94 na senti 42  Januari, mwaka huu ikilinganishwa na Sh 95 na senti 20, ilivyokuwa Desemba, mwaka jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,885FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles