23.9 C
Dar es Salaam
Monday, July 1, 2024

Contact us: [email protected]

Wadaiwa sugu bodi ya mikopo kusakwa zipatikane Sh bilioni 200

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) imezindua kampeni inayolenga kuwasaka wadaiwa ambao hawajalipa mikopo yao tangu walipohitimu masomo.

Kampeni hiyo ijulikanayo kama ‘Fichua’ itaendeshwa kwa miezi miwili ikilenga kukusanya zaidi ya Sh bilioni 200 kutoka kwa wadaiwa zaidi ya 50,000.

Akizungumza leo Juni 28,2024 wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dk. Bill Kiwia, amesema itachochea uwezo wa kutoa mikopo hivyo ili iweze kusaidia kusomesha vijana wengi wa Kitanzania.

“Kampeni hii imelenga wananchi wote, mzazi, mdhamini na wote waliosaini fomu za waombaji mikopo wawafichue vinginevyo watatafutwa wao. Kuna wananchi wamekuwa wanatutumia majina ya wadaiwa na namna wanavyopatikana na baadhi tumewapata wameanza kurejesha,” amesema Dk. Kiwia.

Amewaomba wananchi kuwafichua wadaiwa kwa kutuma majina, eneo wanaloishi, wanakofanyia kazi kupitia barua pepe au kupiga simu namba 0736665533 au kutuma ujumbe wa WhatsApp namba 0739665533

Mkurugenzi wa Uendeshaji na Urejeshwaji wa Mikopo, George Mziray, amesema kasi ya urejeshaji imekuwa ikiongezeka kutoka kukusanya Sh bilioni 2 mwaka 2016 hadi Sh bilioni 15 kwa mwezi.

“Tunafahamu wadaiwa wengi wamemaliza miaka miwili ya matazamio tangu walipomaliza masomo lakini hawajaanza kurejesha, wapo mtaani na wengine wana vipato lakini hawataki kulipa, tutaendelea kuwa wabunifu kwa kuandaa na kutekeleza mikakati rafiki ya kuwafikia wadaiwa wote,” amesema Mziray.

Kampeni hiyo ni mojawapo ya shamrashamra za kuadhimisha miaka 20 ya bodi hiyo tangu ilipoanzishwa mwaka

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles