28.9 C
Dar es Salaam
Friday, July 19, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania tembeleeni Maonyesho ya Sabasaba”-CAG Kichere

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere, ametoa wito kwa wananchi kutembelea Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba ili kujifunza na kufahamu huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi za serikali na binafsi kwa ajili ya kuwahudumia wananchi.

Akizungumza leo, Julai 1, 2024, alipotembelea maonesho hayo yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam, Kichere aliwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi ili kufaidika na elimu na huduma zinazotolewa katika maonesho hayo.

“Hapa nilipo ni banda la Ofisi ya Waziri Mkuu, kuna taasisi zote zilizo chini ya ofisi hiyo. Sasa ni muda wa pekee kwa wananchi kujitokeza, kuja kujifunza na kuhudumiwa hapa na kwenye taasisi nyingine. Nimepata bahati ya kupita kwenye mabanda tofauti na kuona huduma zinazotolewa. Kiukweli ni muhimu kwa wananchi kufika hapa,” alisema Kichere.

Aliongeza kuwa uwepo wa banda la kuwezesha wananchi kiuchumi chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ni fursa kubwa kwa wananchi kujua jinsi wanavyoweza kufikiwa na mipango ya uwezeshaji inayofanywa na ofisi hiyo.

Kichere pia alisifu maboresho makubwa yaliyofanyika kwenye maonesho hayo, akieleza kuwa ni matarajio yake kuona huduma bora zinatolewa na wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki maonesho hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles