26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga yajitosa Dar Boxing Derby

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Uongozi wa klabu ya Yanga, umevutiwa na maandalizi ya pambano ya ngumi ya Dar Boxingi Derby na kuahidi  kutoa mchango wao katika kufanikisha jambo hilo ikiwamo kununua tiketi za VIP.

Hayo yamesemwa na Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ali Kamwe wakati mabondia watakaopanda ulingoni siku hiyo ya Juni 29,2024 kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama, jijini Dar es Salaam walipotembelea  Makao Makuu ya Wanajangwani hao pamoja na waandaji ili kujifunza mambo mbalimbali.

 Kamwe amesema Yanga itaongeza nguvu katika maandalizi ya pambano hilo kutokana na uzoefu wao wa kuandaa derby  ili kuongeza mvuto  na kulifanya pambano hilo litambulike zaidi.

” Yanga ni kati ya klabu ambayo inasapoti mchezo wa ngumi kwa sababu zamani ilikuwepo klabu ya ngumi hapa. Ujio huu wa mabondia kuja kufanya ziara hapa ya kujifunza kwetu, ni mwanzo mzuri wa kuweza kurejesha ┬áklabu ya ngumi Yanga,” amesema Kamwe.

Naye mdau wa ngumi  nchini, Meja Selemani Semunyu, ameishukuru Yanga kwa kupokea ombi la kwenda kujifunza vitu tofauti kutoka kwao, huku akimuomba Rais wa klabu hiyo Mhandisi Hersi Said kutoa sapoti yake hata kwa udhamini kupitia moja ya bidhaa wanazozalisha.

Kwa upande wao mabondia wamefurahishwa na ziara hiyo na kukiri kujifunza vitu vingi na kuahidi kutoa burudani ya masumbwi siku hiyo.

Kati ya mabondia ni Nassib  Ramadhani anayepigana na  Juma Choki ambapo amesema  amejiandaa vizuri kuonyesha mchezo safi kutokana na ukongwe wake, huku akitamba kumfunza  kumfunza adabu mpinzani wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles