28.9 C
Dar es Salaam
Friday, July 19, 2024

Contact us: [email protected]

CAG atoa kongole kwa PPAA

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere ameipongeza Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutoa elimu kwa umma kuhusu majukumu yake.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere akisaini kitabu cha wageni katika banda la Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.

Kichere ametoa pongezi hizo wakati alipotembelea banda la PPAA katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Huduma ya Sheria PPAA, Agnes Sayi akiongea kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa PPAA, James Sando amemueleza CAG kuwa Sheria mpya ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023 imeboresha masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja kupunguzwa kwa muda wa kushughulikia malalamiko na rufaa zinazotokana na michakato ya Ununuzi wa Umma kutoka siku 45 hadi siku 40.

“Mabadiliko ya Sheria ya Ununuzi yamekuwa yakifanyika mara kwa mara kwa lengo la kupunguza muda, kuongeza uwazi na usawa katika shughuli za ununuzi wa umma, kuongeza ushindani,” alisema Sayi

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere akimsikiliza Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Huduma ya Sheria PPAA, Agnes Sayi wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Kadhalika, Sayi ameongeza kuwa PPAA imefanikiwa kuanzisha Moduli ya kushughulikia malalamiko na rufaa kwa njia kieletroniki ambapo moduli hiyo ipo katika mfumo wa ununuzi wa umma kieletroniki (NeST) ambapo kupitia moduli hiyo wazabuni wataawasilisha malalamiko yao kieletroniki jambo ambalo litasaidia kuokoa muda na gharama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles