Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT, Mary Chatanda akikabidhi Msaada Mbalimbali kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama leo Desemba 5, walipowatembelea wakiwa wajumbe wa Kamati ya Maafa ya UWT na Viongozi wa Mikoa ya Manyara na Arusha katika kuwapa pole walioathirika na mafuriko hayo.
Chatanda amesema kwa hakika huu msiba mzito ambao umeshtua Taifa na kila mtu na wao kama Umoja wa wan awakeanawake Tanzania wamejikusanya kwa umoja wao kuleta Msaada huu ambao utasaidia kwa wananchi wa Hanang.Â
“Sisi tulikuwa Rufiji kwenye Tamasha la Kumuenzi Bibititi Mohamed, lakini tukapata taaharifa hii na baadae tukaona kwenye Vyombo mbalimbali vya Habari tukasema kweli hali ni mbaya ndivyo tukaketi na kamati yangu ya Utekelezaji tukaamua tuje na hiki kidogo kwa ajili ya kurejesha tabasamu kwa watu ambao wamepata shida hii,” amesema Chatanda.Â