22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Tunataka namba moja Kitaifa –Shule ya Lusasaro

*Ni baada ya kushika namba tatu mkoa wa Dar

Na Mwandishi Wetu, Mtanzani Digital

Shule ya Msingi Lusasaro iliyoko Tabata Kisukuru Jijini Dar es Salaam imedhamiria kuongoza matokeo ya darasa la saba kitaifa mwakani baada ya kushika nafasi ya tatu mkoa wa Dar es Salaam.

“Tunataka kuongoza kitaifa , uwezo huo tunao kama tumeshika namba tatu Ki-mkoa kwanini isiwe kitaifa? Anahoji Louis Lugata, Mjumbe wa Bodi ya Shule hiyo.

Louis anasema kuwa ushirikiano baina ya mamlaka zinazosimamia Elimu, Waalimu wazazi na wanafunzi ndiyo siri ya mafanikio yao.

Katika matokeo yaliyotangazwa hivi Karibuni na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) kwa Darasa la Saba mwaka 2023 shule hiyo ya Mchepuo wa Kiingereza imeshika nafasi ya tatu ki- mkoa na kuongoza kwenye Kata ya Tabata Kisukuru.

Anasema kuwa wamejiandaa kuzalisha kizazi bora cha wahitimu ambao watakuja kulisaidia taifa siku za baadaye kwa kuibua na kukuza  vipaji vya vijana na hatimaye kuja kuwa viongozi bora.

Naye Mwalimu wa Taaluma shuleni hapo, Maganiko Simon anabainisha kuwa wamedhamiria kuzalisha vijana ambao watakuwa na uwezo wa kufikiri vizuri na wabunifu ambao wataifanya Tanzania kuwa nchi bora.

“Sisi tunataka kuifanya Tanzania kuwa nchi bora kwa kuzalisha vijana ambao wana uwezo wa kufikiri na kuwa wabunifu,” anasema.

Anabainisha kuwa taifa ili liendee linahitaji watu watu wenye ubunifu na hatimaye kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii kwa ubunifu wao.

Shule ina panga kijikita katika kuibua vipaji kwa vijana na kwani Dunia ya sasa vipaji vinalipa sana na kuongeza pato la taifa, watawekeza zaidi katika masomo ya kumpyuta na miundombinu ya michezo mbalimbali anasema Lugata.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles