31.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

Uingereza kuikosa El Clasico Desemba 3

el-clasico-kati-ya-barcelonaMADRID, HISPANIA

WADAU na wapenzi wa soka nchini Uingeraza, watashindwa kuangalia mchezo wa El Clasico kati ya Barcelona ambao watakuwa kwenye uwanja wa nyumbani dhidi ya wapinzani wao Real Madrid.

Inadaiwa kwamba, mchezo huo wa kwanza kuikutanisha miamba hiyo msimu huu utapata nafasi ya kutazamwa moja kwa moja jumla ya nchi 100, lakini watu wa nchini Uingereza watakosa nafasi hiyo kutokana na muda ambao umepangwa mchezo huo kuchezwa.

Mchezo huo umepangwa kupigwa saa 3:15 mchana, wakati sheria za soka nchini Uingereza zinadai kuwa ni ruksa kuonesha mchezo moja kwa moja kuanzia saa 2:45 na saa 5:15 kwa siku ya Jumamosi ambapo mchezo huo utapigwa.

Kutokana na hali hiyo, Uingereza watashindwa kuutazama mchezo huo moja kwa moja (live) na badala yake watatazama matukio yatakayojiri katika mchezo mara baada ya kumalizika.

Inasemekana kuwa Chama cha Soka nchini England (FA) na ligi kuu, waliwahi kukaa na kujadili juu ya sheria hiyo huku wakiwa na maana kwamba kuwafanya mashabiki nchini England wajitokeze kwa wingi viwanjani.

Kwa hali hiyo mashabiki wa nchini Hispania, USA, China na mataifa mengine watafurahia mchezo huo kuutazama moja kwa moja.

Inasemekana kuwa mwaka 2014, mashabiki ambao walikuwa wanaangalia soka kupitia Sky Sports, walishindwa kumuona mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez, katika dakika 15 za mwanzo kutokana na sheria hiyo kuwabana watu wa nchini Uingereza.

Sheria hiyo ilipangwa tangu mwaka 1960, huku wakiwa na lengo la kukusanya mashabiki wengi viwanjani badala ya kuutazama mchezo katika televisheni.

Sheria hiyo iliwekwa na mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Burnley, Bob Lord, ambapo alidai kuwa muda kama huo unawafanya mashabiki kubaki majumbani kuutazama mchezo badala ya kwenda uwanjani siku hiyo ya Jumamosi hivyo pato linakuwa dogo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles