21.9 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Ronaldinho amtabiria Messi Ballon d’Or

messi-ronaldinho-1450907869183BARCELONA, HISPANIA

NYOTA wa zamani wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Brazil, Ronaldo de Assis Moreira ‘Ronaldinho’, amemtabiria mshambuliaji wa klabu hiyo, Lionel Messi, kuwa atachukua tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia 2016, Ballon d’Or.

Ronaldinho, aliwahi kucheza pamoja na mchezaji huyo miaka ya nyuma katika klabu hiyo ya Barcelona kabla ya kujiunga na AC Milan, lakini kwa sasa anaamini kuwa Messi ana nafasi kubwa ya kutwaa uchezaji bora wa dunia katika tuzo ambazo zitatolewa mwakani.

“Kwa sasa Messi ni mchezaji mwenye kiwango cha hali ya juu, amekuwa na mchango mkubwa katika klabu yake hivyo ninaamini katika tuzo za Ballon d’Or 2016, nyota huyo anastahili kutwaa tuzo hiyo.

“Ushindani ni mkubwa sana katika kuwania tuzo hiyo, lakini ukweli ni kwamba mchezaji huyo japokuwa amekuwa na upinzani na Ronaldo, lakini kwa upande wangu Messi anastahili.

“Siku zote napenda kumuona Messi akiwa na furaha, nilikuwa na furaha sana baada ya mchezaji huyo kubadilisha maamuzi na kuamua kurudi kuitumikia timu ya taifa ya Argentina, Messi ni rafiki yangu wa karibu, tunabadilishana mawazo mara kwa mara,” alisema Ronaldinho.

Hata hivyo, Ronaldinho amedai kuwa Messi ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa lakini bado hajafikia uwezo wa wachezaji wa zamani kama vile Maradona na Pele.

“Japokuwa Messi amekuwa na uwezo mkubwa kwa sasa, lakini bado hajafikia uwezo wa nyota wa zamani kama vile Maradona na Pele, wachezaji hao walifanya makubwa katika kipindi chao na kuweka historia kubwa,” aliongeza Ronaldinho.

Hata hivyo, Ronaldinho, aliongeza kwa kumsifia nyota wa sasa wa timu hiyo ya taifa, Neymar, kwamba ni mchezaji ambaye anaweza kuweka historia katika soka la sasa kama ataendelea kujituma na kuonesha nidhamu katika soka.

“Neymar kwa sasa ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa ndani ya kikosi cha Brazil na anaweza kubadilisha matokeo muda wowote, ninaamini siku moja atakuja kuwa mchezaji bora wa dunia kama ilivyo kwa wachezaji wengine.

“Kikubwa ambacho anatakiwa kuangalia kwa sasa ni kuendelea kujituma na kutambua nini anatakiwa kukifanya ili kuweza kutimiza malengo yake, anafanya makubwa akiwa na Messi, Iniesta ndani ya klabu ya Barcelona, wachezaji hao wananifanya niwe na furaha nikiwaona vile ambavyo wanavifanya na kuipa ushindi klabu yao,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,719FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles