PARIS, Ufaransa
VIONGOZI mbalimbali duniani wanatarajia kuwasili nchini hapa kushiriki wiki nzima ya kumbukumbuku za Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia kuanzia jana.
Kwa mujibu wa taarifa iliyololewa na Serikali, Rais Emmanuel Macron anajiandaa kuwapokea viongozi zaidi ya 80 ambao watashiriki wiki hii ambako atakuwa mwenyeji wa viongozi akiwamo Rais wa Marekani, Donald Trump na mwenzake wa Urusi, Vladmir Putin.
Mbali na kuwapokea viongozi hao, pia Rais Macron atafanya ziara kaskazini mwa nchi akitembelea maeneo yaliyohushudia mapambano yaliyosababisha vifo vya maelfu ya wanajeshi m kwenye mitaro.
Tarifa hiyo ilieleza kiongozi huyo atatumia fursa hiyo ya kimataifa kutoa onyo dhidi ya kuongezeka kwa siasa kali za umaarufu mbele ya Trump anayendeleza sera ya “Marekani Kwanza” na viongozi wengine wa siasa za uzalendo.
Maadhimisho hayo yatafikia kilele chake katika sherehe itakayofanyika katika lango la Arc de Triomphe mjini hapa, Novemba 11 mwaka huu na kuhudhuriwa na viongozi kadhaa akiwamo Trump, Putin na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, miaka 100 tangu kusainiwa makubaliano ya kuacha mapigano.
Hafla katika eneo la mnara wa Kaburi la Mwanajeshi Asiyejulikana kwenye mtaa wa Champs-Elysees itafanyika huku kukiwa na ulinzi mkali kutokana na mfululizo wa mashambulio makali ya wanamgambo wa itikadi kali nchini hapa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Maadhimisho yalianza jana kwa tamasha la muziki linaloadhimisha urafiki kati ya maadui wawili wa zamani wakati wa vita, Ufaransa na Ujerumani, katika mji wa mpakani wa Strasbourg, ambalo lilihidhuriwa na Rais Macron na Rais wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier.
Pia kwa mujibu wa ratiba ya hafla hiyo, Rais Macron atatumia wiki nzima kuyatembelea maeneo yaliyoshuhudia mapambano katika upande wa magharibi, kutoka Verdun hadi Somme.
hayo yanayotokea ufaransa_ni historia tosha katika dunia yetu ya sasa, kama dunia viongozi wetu wa sasa wajifunze matatizo yatokanayo na vita! vita visimamisho kote dunia kwa sasa!