24.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Kiongozi wa upinzani Cameroon  ataka kura zihesabiwe upya

AYOUNDE, Cameroon

MGOMBEA urais wa upinzani nchini hapa, Maurice Kamto, ametaka  kura katika uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita zihesabiwe upya na ameitka Jumuiya za Kimataifa kuchukua jukumu hilo.

Kwa mujibu wa matokeo ya kura hizo, Kamto alishika nafasi ya pili baada ya kupata asilimia  14.23 ya kura nyuma ya Rais  Paul Biya.

Katika madai yake hayo juzi, Kamto, ambaye alijitangazia ushindi siku moja kabla ya matokeo ya uchaguzi huo wa Oktoba 7 kutangazwa,anahoji kitendo cha kucheleweshwa wiki kadhaa kabla ya mshindi kutangazwa zilikuwa njama za serikali kuchakachua matokeo.

Alisema mbali na kuchelewa kutangazwa matokeo, pia kazi ya kuhesabu kura hizo ilijaa mizengwe na akasema  kitendo cha Baraza la Katiba kumtangaza Rais  Biya kuwa ndiye mshindi hakubaliani nacho.

“Kamwe hatuwezi kuyakubali  matokeo yaliyotangazwa na Baraza la Katiba,” alisema na kuongeza kwamba atapiga kampeni kwa amani dhidi ya matokeo rasmi.

Kamto (64) ambaye ni mwanasheria na kiongozi wa Chama cha  MRC, aliwataka wapinzani wenzake kuungana naye  kuendesha kampeini hiyo ya kupinga matokeo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,074FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles