25.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Ufaransa yaadhimisha karne ya     ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia

PARIS, Ufaransa

VIONGOZI mbalimbali duniani wanatarajia kuwasili nchini hapa kushiriki  wiki nzima  ya  kumbukumbuku za Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia kuanzia   jana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyololewa    na Serikali,  Rais Emmanuel Macron anajiandaa kuwapokea viongozi zaidi ya 80 ambao  watashiriki wiki  hii  ambako atakuwa mwenyeji wa viongozi akiwamo Rais wa Marekani, Donald Trump na mwenzake wa Urusi, Vladmir Putin.

Mbali na kuwapokea viongozi hao, pia Rais Macron atafanya ziara kaskazini mwa nchi  akitembelea maeneo yaliyohushudia mapambano  yaliyosababisha vifo vya maelfu  ya wanajeshi m  kwenye mitaro.

Tarifa hiyo ilieleza kiongozi huyo atatumia fursa hiyo ya kimataifa kutoa onyo dhidi ya kuongezeka kwa siasa kali za umaarufu  mbele ya Trump anayendeleza sera ya “Marekani Kwanza” na viongozi wengine wa siasa za uzalendo.

Maadhimisho hayo yatafikia kilele chake katika sherehe itakayofanyika katika lango la Arc de Triomphe mjini hapa, Novemba 11 mwaka huu  na kuhudhuriwa na viongozi kadhaa akiwamo Trump, Putin na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, miaka 100 tangu kusainiwa makubaliano ya kuacha mapigano.

Hafla katika eneo la mnara wa Kaburi la Mwanajeshi Asiyejulikana kwenye mtaa wa Champs-Elysees itafanyika huku kukiwa na  ulinzi mkali kutokana na mfululizo  wa mashambulio makali ya wanamgambo wa itikadi kali nchini hapa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Maadhimisho yalianza jana kwa tamasha la muziki linaloadhimisha urafiki kati ya maadui wawili wa zamani wakati wa vita, Ufaransa na Ujerumani, katika mji wa mpakani wa Strasbourg, ambalo lilihidhuriwa na Rais  Macron na Rais wa Ujerumani,  Frank-Walter Steinmeier.

Pia kwa mujibu wa ratiba ya hafla hiyo, Rais Macron atatumia wiki nzima kuyatembelea maeneo yaliyoshuhudia mapambano katika upande wa magharibi, kutoka Verdun hadi Somme.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,213FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles