27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

UDIWANI KWA MANJI FIGISU ZATAWALA

PATRICIA KIMELEMETA, DAR ES SALAAM


WAGOMBEA udiwani wa vyama vya CUF, Chadema na Ada-Tadea, wamelalamikia hatua ya msimamzi wa uchaguzi Kata ya Mbagala Kuu, kumtangaza mgombea wa CCM kupita bila kupingwa ingawa  wamerejesha fomu kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza na MTANZANIA jana, mgombea wa CUF, Abukabar Mlawa, alisema hatua ya kutangazwa mgombea wa CCM, Shabani Abubakar ni  kinyume na sheria za uchaguzi.

Awali, kata hiyo ilikua inaongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuph Manji ambaye aliondolewa kwa mujibu wa sheria baada ya kuonekana ameshindwa kuhudhuria vikao vya baraza la madiwani kwa muda mrefu.

Mlawa alisema  jana kuwa msimamizi wa uchaguzi wa kata hiyo aliwataka wagombea wa vyama mbalimbali kuchukua fomu za kuwania udiwani kuanzia Agosti 17, mwaka huu na kutakiwa kuzirudisha fomu hizo jana saa 10:00 jioni.

Alisema ilipofika saa 5:00 asubuhi jana, yeye pamoja na wagombea wa vyama vingine vya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), ACT-Wazalendo na CCM, walirudisha fomu hizo   lakini ilipofika saa 10:00 jioni walikuta msimamizi huyo ameshampitisha mgombea wa CCM.

Alisema kitendo hicho kimewashangaza kwa sababu sheria za uchaguzi hazijafuatwa, jambo ambalo limesababisha kujitokeza   malalamiko.

Naye mgombea wa Chadema, Muganyizi Emanuel alisema walirudisha fomu saa 5: 00 asubuhi wakati muda uliotangazwa wa mwisho ni saa 10:00 jioni, lakini walishangazwa na kitendo cha msimamizi msaidizi wa uchaguzi kumpitisha mgombea bila ya kufuata sheria.

Mgombea wa Ada-Tadea, Alicidia Zabibu alisema   walifuata taratibu zote za malipo kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke kama sheria invyowataka.

Alisema kinachowashangaza ni kuona msimamizi msaidizi wa uchaguzi wa kata hiyo kukataa kuchukua fomu yao kwa madai kuwa walichelewa kurudisha.

Alipoulizwa,  Msimamizi Msaidizi wa Kata hiyo, Elias Joseph alisema   suala hilo atalitolea ufafanuzi leo.

“Kwa sasa siko sehemu nzuri, ila naomba nitafute kesho(leo)  niweze kutoa ufafanuzi kuhusiana na suala hilo,”alisema Joseph.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles