29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

BOBI WINE AACHIWA, AKAMATWA TENA KWA UHAINI

KAMPALA,Uganda


MBUNGE wa Jimbo la  Kyadondo lililopo Mashariki mwa nchi hii,  Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine amefunguliwa mashitaka ya uhani, baada ya kukamatwa  muda mfupi baada ya mahakama ya kijeshi kumwondolea mashitaka ya kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Wine alikamatwa upya na kushtakiwa katika mahakama ya hakimu mkuu kujibu mashtaka ya uhaini pamoja na wabunge wengine kadhaa.

Mbunge huyo ambaye pia ni mwanamuziki jana alifikishwa katika mahakama ya kijeshi iliyopo mjini Gulu Kaskazini mwa Uganda.

Kabla ya kufikishwa mahakamani, awali mawakili wake walielezwa kuwa  kesi hiyo itasikilizwa katika kambi ya kijeshi ya Makindye iliyopo jijini hapa ambako anashikiliwa.

Kumekuwa na shinikizo kubwa kimataifa la kutaka Bobi Wine aachiwe huru na wananchi wengi wa hapa   wanaitazama kesi hii kama jitihada za kumnyamazisha mkosoaji mkuu wa serikali aliyechaguliwa kuwa mbunge mwaka jana.

Wakili wa  jeshi wameeleza mahakama kuwa mashtaka dhidi ya Wine yameondolewa na kwamba mwanasiasa huyo akabidhiwe kwa polisi ili akabiliwe na mashtaka ya uhaini pamoja  na wabunge wengine waliokamatwa .

Wakili wa mbunge huyo, Medard Segona aliiambia mahakama kwamba licha ya kuwa wameridhishwa na hatua ya mahakama ya kijeshi , anapinga hatua ya sasa ya mteja wake kuhamishwa katika mahakama ya kiraia kukabiliwa na mashtaka mapya.

Alitaka mbunge huyo aachiwe huru ili aweze kupelekwa kupokea matibabu, lakini wakakataliwa  kwa kile kilichodaiwa na mahakama kuwa  mbunge huyo angweza kuachiwa huru kama kusingekuwapo na kosa jingine ambalo linamkabili.

Jitihada za kumshtaki mbunge huyo  mbele ya mahakama ya kijeshi zimekabiliwa na shutuma kubwa kimataifa na hata miongoni mwa makundi ya kutetea haki za binadamu.

Nchini Kenya, raia walimiminika katika mji mkuu wa Nairobi  jana  kushinikiza kuachiwa kwa mbunge huyo wa upinzani na huku mjini hapa polisi imemkata kiongozi mkuu wa upinzani Kizza Besigye.

Besigye alikamtwa mapema jana  wakati alipojaribu kuondoka nyumbani kwake Kasangati; na inataarifiwa kuwa  amefikishwa katika kituo cha polisi cha Naggalama.

Wasanii waja juu

Katika hatua nyingine , Wanamuziki wakubwa wakiwemo Chris Martin , Angelique Kidjo na Damon Albarn, wametoa wito wa kuachiwa kwa mbunge huyo  ambaye ana wiki sasa tangu kukamatwa kwake na mbunge mwezake na zaidi ya watu 30. Wasanii hao wamejaza waraka wa kutaka mbunge huyo wa upinzani kuachiwa huru.

Wakili aichongea Serikali kwa Marekani

Mmoja wa mawakili ambaye amewaajiri kutoka Marekani  Robert Amsterdam alisema kukamatwa mteja wake kumechochewa kisiasa na ni kitendo cha dhuluma na kuongeza kuwa ameteswa akiwa kizuizini madai ambayo yanakanushwa, huku Rais Yoweri Museveni akiyataja madaia hayo ni ya  uongo.

Amsterdam alisema Marekani inastahili kuwawekea vikwazo maofisa wa  hapa  akiongeza kuwa ni lazima wafahamu kuwa kuna majibu kwa ukiukaji huu wa haki za binadamu.

Alieleza kuwa Sheria za Marekani zinazofahamika kama Magnitsky zinaruhussu Bunge la Congress kuwawekea vikwazo wale wanaokiuka haki za binadamu popote pale duniani.

Mbunge huyo na wengine kadhaa wanashikiliwa tangu wiki iliyopita wakati wakiwa katika mkutano wa  katika Jimbo la  Arua  lililopo kaskazini Uganda.

Bobi Wine ni nani?

Nyota huyo wa mtindo wa Afrobeats aliingia katika taaluma ya muziki miaka ya 2000 na anaelezea kipaji chake kuwa ni cha kuelimisha na kuburudisha. Mojawapo ya vibao vyake vya awali Kadingo, inahusu usafi wa mwili.

Jina lake kamili ni Robert Kyagulanyi Ssentamu, alichaguliwa kuwa mbunge katika uchaguzi mdogo baada ya kusimama kama mgombea huru mwaka jana wilayani Kyadondo Mashariki mwa ya nchi.

Aliwashinda wagombea kutoka chama tawala National Resistance Movement (NRM) na chama kikuu cha upinzani Democratic Change (FDC).

Baada ya kutangazwa mshindi, aliahidi kujitahidi  kuwaunganisha raia. “Jambo langu la kwanza ninalotaka kufanya ni kufanikisha maridhiano kati ya viongozi wa Kyadondo Mashariki…Ninataka siasa zitulete pamoja… jinsi muziki ufanyavyo,”alisema mara baada ya kuchaguliwa

Kigogo huyo anatarajiwa kufikishwa katika mahakama ya kiraia Agosti 30 mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles