26.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Uchaguzi Congo uko pale pale

Kinshasa, Congo

Licha ya kuzuka kwa moto ulioteketeza majengo yanayotumiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (CENI), mjini Kinshasa ambapo unadaiwa kuathiri majengo hayo ambayo yamekuwa yakitumiwa kuhifadhi vifaa vya uchaguzi, uchaguzi nchini humo uko pale pale.

Moto huo ulizuka saa nane usiku wa kuamkia leo Alhamisi Desemba 13,  chanzo chake hakijajulikana, umezua taharuki ikizingatiwa kwamba zimesalia siku 10 uchaguzi mkuu ufanyike nchini humo.

Msemaji wa CENI, Jean Pierre Kalamba,  amenukuliwa na vyombo vya habari akisisitiza licha ya tukio hilo, uchaguzi utafanyika Desemba 23 kama ulivyopangwa.

“Tunatumai kwamba kisa hiki hakitavuruga mchakato wa uchaguzi na uchunguzi unaendelea,” amesema Kalamba.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo, Henri Mova Sakanyi, amesema uharibifu uliotokea ni mkubwa mno bila kutaja vitu vilivyoathirika na moto huo wala thamani yake.

Licha ya wahusika kutotaja vitu vilivyoathirika na moto huo, inadaiwa kulikuwa na mashine zaidi ya 7,000 za kupigia kura ambazo zimeharibiwa na moto huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles