27.8 C
Dar es Salaam
Monday, December 6, 2021

Aweso amsweka ndani mhandisi wa maji kwa kushindwa kukamilisha mradi

Oscar Assenga, Pangani

Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, ameliamuru Jeshi la Polisi wilayani Pangani kumuweka ndani Mhandisi wa Maji wilayani hapo, Novat Wilson, kwa kushindwa kusimamia na kukamilisha kwa wakati
mradi wa maji katika Kijiji cha Mseko wenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 80.

Aweso ametoa agizo hilo jana wakati wa ziara yake baada ya kutembelea katika vijiji vya Mseko na Mafisi na kubaini uwepo wa ubadhirifu wa fedha hizo za Serikali zilizotumwa Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa ajili ya mradi huo huku waliopewa dhamana wakishindwa kuutekeleza.

“Fedha hizo zilitengwa kwa ajili ya vijiji hivyo viwili ambapo kulitakiwa kujengwa vituo vitatu vya maji kwa ajili ya wananchi ambao
wanakabiliwa na adha ya maji kwa muda mrefu jambo ambalo halikutekelezwa kama kusudio la fedha hizo.

“Napata mashaka sana na usimamizi wa hii miradi ikiwa mmeomba fedha na wizara imewaletea mmejenga kituo kimoja tu kama geresha na si kusudio, mafundi wanadai na benki hamna shilingi hata moja nitaelewa nini, maana yake fedha zimeliwa?”amehoji Aweso.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,340FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles