22.4 C
Dar es Salaam
Friday, May 17, 2024

Contact us: [email protected]

Twiga Stars yakabidhiwa kitita cha Rais Samia

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa    ameikabidhi timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars kitita cha sh. 10 milioni ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan baada ya  kuifunga Ivory Coast na kusonga mbele katika kusaka tiketi ya kushiriki  Kombe la Mataifa Afrika(Wafcon 2014).

Twiga Stars iliitoa Ivory Coast   kwa penalty 4-2 katika mchezo uliopigwa wiki iliyopita kwenye dimba la Azam Complex.

Akikabidhi fedha hizo leo Oktoba 2, 2023, jijini Dar es Salaam, Msigwa amesema  Serikali ipo pamoja na wachezaji hao kutokana na kazi kubwa  wanayofanya ya kuiwakilisha nchi kimataifa.

“Mnapokuwa uwanjani katika mechi za kimataifa mnakuwa mmebeba matumaini ya watanzania, katika mechi zote mlizocheza tumeona dhamira mliyonayo kwa nchi yenu, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anawapongeza sana, anafurahi sana anapowaona mnacheza uwanjani, anafurahi sana mnapopata matokeo mazuri katika mechi zetu,” amesema Msigwa.

Kwa upande wake Kocha Mkuu wa timu hiyo, Bakari Shime amesema amefurahi kupokea kiasi hicho cha fedha kutoka kwa Rais Samia kuhamasisha vijana hao kujituma zaidi kupambania nchi yao.

“Fedha ni sehemu kubwa ya hamasa, kitendo cha Rais Samia kuwafuatilia vijana wetu na kutambua timu hiyo inacheza ni faraja kubwa kwao na imekuwa chachu ya kujituma wakiamini kuwa mama yupo pamoja nao,” amesema Shime.

Naye nahodha wa Twiga Stars, Joyce Lema amesema wanamshukuru Rais Samia kwa kuzidi kuwapa hamasa na kumuahidi  kutomuangusha katika mashindano yote yaliyopo mbele yao.

“Kwa hamasa hii inaonyesha kuwa kuna kitu kimeongeza katika soka na wanawake, tunatamani siku moja viongozi kuendelea kujitokeza kwa wingi kusapoti soka la wanawake kama ilivyo kwa wanaume,” amesema Joyce.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles