26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

TPA yatwaa tuzo ya mwajiri bora 2023

Na Mwandishi Wetu

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imetwaa tuzo ya mwajiri bora wa mwaka 2023 kwa taasisi za umma hapa nchini.

Akipokea tuzo hiyo Desemba 4,2023 jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, Meneja Rasilimali Watu wa TPA, Said Msabimana amesema kwamba mafanikio hayo hayakuja  kwa bahati mbaya bali yametokana na mifumo bora ya uajiri waliojiwekea kama TPA.

“Huu ni mwaka wa pili mfululizo kwa TPA, kutwaa tuzo hizo zinazoandaliwa na kusimamiwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na kufanyika kila mwisho wa mwaka,” amesema Msabimana.

Kwa mujibu wa wandaaji wa tuzo hizo, lengo la kuanzishwa kwake ni katika harakati za kutambua wanachama wanaofanya vizuri katika kuweka mikakati bora yenye kuthamini usimamizi wa rasimali watu na shughuli za biashara.

Tuzo ya mwajiri bora wa mwaka imeendelea kuwa tukio muhimu linalotambulika katika ngazi ya kitaifa ambapo kwa miaka kadhaa sasa tuzo hizi zimehamasisha waajiri kuweka sera bora za ajira na usimamizi wa rasilimali watu.

Mkurugenzi Mkuu wa ATE, Suzanne Ndomba amesema wakati wa utoaji wa tuzo hizo kuwa zimeweza kuchochea na kuongeza tija, mahusiano bora mahala pa kazi, utii wa sheria na ushindani kibiashara.

Akizungumzia mchakato mzima ulivyokuwa, Ndomba amesema makampuni shiriki yaliwasilisha madodoso mawili yaliyojazwa, moja likiwa limejazwa na uongozi au mkurugenzi mkuu au mkuu wa kitengo cha usimamizi wa Rasilimali Watu na dodoso jingine likiwa limejazwa na mwajiriwa wa kawaida au mwakilishi wa Chama cha Wafanyakazi.

Kwa mwaka huu, uzinduzi rasmi wa mchakato wa kutafuta mwajiri bora wa mwaka wa 2023 ulifanyika Mei 30,2023.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles