31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

TIMBULO: MAJUNGU, FITINA NI CHANGAMOTO KUBWA

Na JENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM



MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Ally Timbulo ‘Timbulo’, amesema vitu alivyovishuhudia vikiongezeka kwa kasi mwaka huu nje ya muziki, ni majungu na fitina.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Timbulo alisema licha ya kupiga hatua katika kazi zake anazofanya, majungu na fitina vimekuwa vikimpa changamoto kubwa.

Timbulo alisema kwa namna moja au nyingine, vitu hivyo vimekuwa vikimpa nguvu ya kuendelea kujituma ili kuhakikisha muziki wake unapiga hatua zaidi.

“Majungu na fitina vimekuwa changamoto kwangu, yani hivi ndivyo vitu ninavyoweza kusema nimeshuhudia vikikua kwa kasi sana mwaka huu,” alisema Timbulo.

Msanii huyo anatarajia kuachia wimbo wa kufungua mwaka, Desemba mwaka huu, ambapo kwa sasa ameanza maandalizi kuhakikisha anakamilisha kazi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles