24.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 17, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania kuiunga mkono Saudi Arabia Expo 2023

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeahidi kuiunga mkono Saudi Arabia kuwa mwenyeji wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara mwaka 2030 (EXPO 2030).

Ahadi hiyo imeelezwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Samwel Shelukindo alipoelezea yaliyojiri katika mkutano kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan na Mjumbe Maalum wa Mfalme wa Saudi Arabia, Ahmed Abdulaziz Qattan uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Balozi Shelukindo amesema katika kikao hicho, Rais amemhakikishia mjumbe huyo maalum kuwa Tanzania itashiriki mkutano ya Nchi za Kiarabu na Afrika (Afro Arab Summit) na Mkutano kati ya Saudi Arabia na Nchi za Afrika itakayofanyika Jijini Riyadh mwezi Novemba 2023.

“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amemhakikishia mjumbe huyo Maalum kuwa Tanzania itaiunga mkono Saudi Arabia kuwa mwenyeji wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya mwaka 2030 alisema Dk. Shelukindo.

Balozi Shelukindo pia aliongeza kuwa Rais amemhakikishia mjumbe huyo kuwa Tanzania itashiriki Mkutano kati ya Nchi za Kiarabu na Afrika (Afro Arab Summit) na Mkutano kati ya Saudi Arabia na Nchi za Afrika inayotarajiwa kufanyika jijini Riyadh, Saudi Arabia mwezi Novemba 2023.

Naye Mjumbe Maalum wa Mfalme wa Saudi Arabia, Mhe. Ahmed Abdulaziz Qattan amesema Saudi Arabia inaishukuru Serikali ya Tanzania kwa kukubali kuiunga mkono kuwa mwenyeji wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya mwaka 2030 (EXPO 2030)

“Kwa niaba ya Serikali ya Saudi Arabia tunaishukuru sana Serikali ya Tanzania kwa kuahidi kutuunga mkono kuwa mwenyeji wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya mwaka 2030 (EXPO 2030),” alisema Qattan.

Aliongeza kuwa Saudi Arabia inamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kitendo cha kukubali Tanzania ishiriki katika Mikutano kati ya Nchi za Kiarabu na Afrika (Afro Arab Summit) na Mkutano kati ya Saudi Arabia na Nchi za Afrika itakayofanyika Jijini Riyadh mwezi Novemba 2023

“Kwa niaba ya Serikali ya Saudi Arabia namshukuru Mheshimwa Rais kwa kukubali kutuunga mkono kuwa mwenyeji wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya EXPO 2030 na kukubali kushiriki mikutano kati ya Nchi za Kiarabu na Afrika (Afro Arab Summit) na Mkutano kati ya Saudi Arabia na Nchi za Afrika itakayofanyika jijini Riyadh mwezi Novemba 2023,” aliongeza Qattan.

Amesema katika kikao hicho wamejadili pia masuala mbalimbali yanayolenga kuimarisha ushirikiano kati ya Saudi Arabia na Tanzania katika nyanja mbalimbali.

Tanzania na Saudi Arabi zimekuwa na uhusiano mzuri na zimekuwa zikishirikiana katika sekta mbalimbali hususan utalii, biashara za bidhaa za nyama, matunda na mazao mengine ya chakula.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles