Derick Milton, Simiyu.
Uongozi wa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu umesema kuwa kuanzia mwezi Desemba mwaka huu mazao yote ya Pamba, Dengu, Choroko, Alzeti na Mbaazi yatanunuliwa kwa mfumo wa stakabadhi Ghalani.
Uhamuzi huo umetangazwa leo na Mkuu wa Wilaya hiyo Festo Kiswaga wakati akiongea na viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika (Amcos) ambapo amesema baada ya muda huo hakuna ununuzi wa mazao hayo holela utafanyika tena.
Kiswaga amesema kuwa kwa sasa wafanyabishara wananunua mazao hayo mitaani huku wakulima wakipata bei ambazo siyo rafiki kwao, ambapo ameeleza kwa mfumo huo bei zitakuwa nzuri kwa wakulima.
” Wanunuzi wa mazao hayo kuanzia leo waanze kujipanga, kuanzia mwezi Desemba mazao yote yatanunuliwa kwenye Amcos kwa kutumia mfumo wa Stakabadhi ghalani, hakutakuwa na nafasi tena ya ununuzi holela tena,” Amesema Kiswaga….
” Kwa sasa wanunuzi wote waanze kujipanga, mazao yote hayo yatanunuliwa kutoka Amcos, lazima tutekeleze maagizo Waziri Mkuu, mfumo wa stakabadhi ghalani, Baada ya Desema marufuku kununua mazao mitaani,” Ameeleza Kiswaga.