25.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

SPIKA NDUGAI APOKEA BARUA YA KALANGA KUJIUZULU

 

|Mwandishi Wetu, Dar es Salaam



Spika wa Bunge, Job Ndugai, amesema amepokea barua ya kujivua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kujiuzulu nafasi ya ubunge kwa aliyekuwa Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Bunge, kutokana na barua hiyo Spika Ndugai amemuandikia barua Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Jaji Semistocles Kaijage kumfahamisha kuwa jimbo hilo liko wazi kwa sasa.

“Mheshimiwa Spika ameandika barua hiyo kwa mujibu wa kifungu cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi (Sura ya 343, ya mwaka 2015), kinachoelekeza kwamba pale ambapo mbunge atajiuzulu, atakufa au sababu nyingine yoyote na zilizoainishwa katika kifungu cha 113.

“Spika atamjulisha Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya  Uchaguzi na kutangaza kwenye Gazeti la Serikali kwamba kiti hicho cha ubunge kiko wazi,” imesema taarifa hiyo.

Aidha, kutokana na barua hiyo, NEC inaweza kuendelea na mchakato wa kumpata mbunge wa kujaza nafasi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles