Derick Milton, Simiyu.
Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO), Pro.Silvester Mpanduji amesema wamejipanga kutoa mafunzo kwa wajasiliamali wote nchini jinsi ya kutengeneza mifuko mbadala.
Prof Mpanduji amesema hayo leo Mei 29,mkoani Simiyu, wakati wa makabidhiano ya ofisi ya Sido Mkoa hapo pamoja na mkandarasi SUMA JKT baada ya kukamilisha ujenzi wake yaliyofanyika mtaa wa Kidulya mjini Bariadi.
Amesema katika kuelekea kuanza kwa utekelezaji wa katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki,shirika hilo litahakikisha wanatoa fursa kwa kila mjasiliamali kujifunza namna ya kutengeneza mifukohiyo.
“kwa sasa tumeanza Mkoa wa Dar es Salaam kutoa mafunzo na baadae tutaendelea kutoa mafunzo hayo kwa mikoa mingine ambayo ina ofisi za Sido…na kwa sasa watafundishwa kutengeneza kwa kutumia mikono huku tukisubiri mashine”Prof Mpanduje.
Akitoa taarifa ya ujenzi wa ofisi hiyo meneja wa SUMA JKT kanda ya Ziwa Luten Kanal Petro Ngata ameishukuru Sido kwa kuwaamini na kuwapatia zabuni ya ujenzi wa ofisi huo ambao umekamilika kwa asilimia 100.