25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Miradi 88 yajengwa chini ya kiwango

Ramadhan Hassan,Dodoma

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa, amesema miradi 88 nchini imejengwa chini ya kiwango kati ya mwaka 2010 na 2015.

Mbarawa amesema hayo leo Mei 29,  wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu(Chadema).

Katika swali lake Komu amesema  kuna miradi imejengwa chini ya kiwango na kusababisha wananchi kutaabika kwa kukosa maji na kuhoji ni hatua gani ambazo serikali imechukua.

Akijibu swali hilo la nyongeza, Waziri Mbarawa alikiri kuwepo kwa miradi ya maji iliyojengwa chini ya viwango na kuongeza kuwa kati ya mwaka 2010 na 2015 miradi 88 nchini nzima ilijengwa chini ya kiwango.

Amesema nia ya serikali ni kuhakikisha wananchi wake wanapata maji, hivyo hatua ya kwanza imekuwa ikikarabati vyanzo hivyo vya maji na kwamba imetengwa Sh milioni 135 kwa ajili ya ukarabati wa miradi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles