27.4 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

TCRA yalenga kuimarisha usalama

Amina Omari, Tanga

Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA imesema usajili wa line za simu za Mkononi umelenga kuimarisha usalama na kupata taarifa sahihi za watumiaji

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 29, Jijini Tanga, Kaimu Mkuu wa TCRA Kanda ya Kaskazini , Mhandisi Imelda Salum amesema hayo kwenye maonesho ya Saba ya biashara kimataifa yaliyofanyika Mkoani hapo.

Amesema usajili huo ambao unafanyika kwa njia ya kieletroniki utasaidia kupata taarifa sahihi za watumiaji wa mitandao ya simu

“usajili huo utaweza kuweka mifumo rahisi kwa watoa huduma kujua idadi kamili ya wanaowahudumia

Hata hivyo aliwatoa hofu wananchi kuwa zoezi Hilo lipo kisheria na kwamba wasiweze kuwa na hofu bali wahakikishe wamezisajili laini zao

Amesema usajili huo pia unalengo la kuwabaini matapeli na wanaotumia Mawasiliano ya simu vibaya kuweza kuwadhibi kwa urahisi

“Kama Sasa kuna wizi wa kimitandao lakini Mara baada ya mfumo wa usajili k ukamilika wataweza kuwabaini haraka watu hao na kuwa fikisha kwenye vyombo vya sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles