Serikali imeadhimia kupanga ada elekezi kwa vyuo vikuu vya Afrika Mashariki ili kuiboresha elimu ya Tanzania iweze na kuondoa tabia ya kukimbilia nje kutafuta elimu.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Mwinyi amesema, uwepo wa ada elelezi utaleta usawa kwa wahitimu wa vyuo vikuu katika soko la ajira la Afrika Mashariki.
Amesema imekuwa kawaida kukimbilia nje kutafuta elimu hali ambayo inasababisha baadhi ya watu kuona kama elimu ya hapa nchini haina hadhi.
Balozi Mwinyi alisema ili kuirejeshea thamani elimu ya Tanzania wameamua kuweka ada maalum itakayotumika katika vyuo vyote vya Afrika mashariki .