23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

IBRAHIMOVIC APEWA TUZO MCHEZAJI BORA SWIDEN

STOCKHOLM, SWIDEN


 

zlatanCHAMA cha soka nchini Swiden, FA (SvFF), kimemtunukia zawadi Zlatan Ibrahimovic ya kuwa mchezaji bora wa mwaka katika timu ya taifa.

Sherehe za utoaji wa tuzo hiyo ilifanyika nje ya Uwanja wa Friends Arena, uliopo mji mkuu wa nchi hiyo.

Mchezaji huyo amefanikiwa kupewa tuzo ya mpira wa dhahabu kwa ajili ya uchezaji bora wa timu ya taifa, pamoja na tuzo ya mchezaji bora wa kiume kwa miaka 10 mfululizo.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 36, ambaye kwa sasa anakipiga nchini England kwenye klabu ya Manchester United, alikuwa na mchango mkubwa ndani ya timu ya taifa ambapo hadi kumalizika kwa michuano ya Euro 2016, mchezaji huyo alikuwa amecheza jumla ya michezo 116 huku akifunga mabao 62 kabla ya kutangaza kustaafu.

Chama hicho kitaendelea kumkumbuka mchezaji huyo hasa kutokana na historia aliyoiweka ndani ya ofisi za chama hicho hasa pale alipoifunga England mabao manne peke yake huku timu hiyo ikishinda mabao 4-2 katika mchezo wa kufungua Uwanja wa Friends Arena mwaka 2012 nchini Swiden.

Ibrahimovic ni mchezaji wa pekee katika timu hiyo ya taifa kuongoza kwa tuzo, ambapo hadi sasa amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo ya mpira wa dhahabu mara 11 tangu aanze kuitumikia timu hiyo mwaka 2001.

Mchezaji huyo alikishukuru chama hicho kwa mchango wake wa kumfanya awe hapo kwa sasa, pia aliwashukuru mashabiki wake wote ambao walikuwa nyuma yake ndani ya timu hiyo kwa kipindi chote.

“Najua kuna wakati watu wanajiuliza kwanini mimi? Lakini kuna wakati naangalia safari yangu ya soka kwa miaka 15 ndani ya timu ya taifa na miaka 20 kwenye klabu, ni wazi kwamba nimefanya makubwa na nastahili kupewa pongezi.

“Wengine wanapewa tuzo kama hizi baada ya kufa, lakini kwa upande wangu ninafuraha kwa kuwa ninapewa tuzo huku nikiwa hai na ninaamini nikifa kumbukumbu zitaendelea kuwepo,” alisema Ibrahimovic.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles