23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Ronaldo: Griezmann hanipendi hata kidogo

MADRID, HISPANIA


cristiano-ronaldo-antoine-griezmannMSHAMBULIAJI wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo, amedai kuwa aliwahi kuambiwa na nyota wa klabu ya Atletico Madrid, Antoine Griezmann, kuwa hampendi hata kidogo.

Wawili hao walikutana katika mchezo wa fainali ya michuano ya Kombe la Euro 2016, ambapo timu ya taifa ya Ureno ilifanikiwa kutwaa taji hilo mbele ya wenyewe Ufaransa kwenye uwanja wa nyumbani.

Ronaldo na Griezmann kila mmoja alitarajia kuisaidia timu yake lakini Ronaldo alifanikiwa kutoa mchango mkubwa ndani ya uwanja hadi nje, mara baada ya kutoka katika dakika 45 za kipindi cha pili kutokana na kusumbuliwa na goti ambapo mchango wake ulikuwa kama kocha.

Ronaldo baada ya kuchukua ubingwa huo, alikwenda Miami nchini Marekani kwa ajili ya mapumziko, hivyo alikutana na Griezmann katika mgahawa akipata chakula na rafiki zake na ndipo mchezaji huyo aliinuka na kumfuata Ronaldo na kumwambia kuwa anamchukia.

“Lilikuwa jambo la kufurahisha,” Ronaldo aliambia France Football. “Kwa sababu muda mfupi mara baada ya kumalizika kwa michuano ya Euro 2016, nilikwenda Miami kwa ajili ya mapumziko, nilikutana na Antoine Griezmann kwenye mgahawa akiwa na rafiki zake wakipata chakula. Alikuja hadi nilipo, huku akiwa anatabasamu na kuniambia Cristiano, nakuchukia,’ alisema Ronaldo.

Hata hivyo, mchezaji huyo alikumbushia jinsi alivyojisikia baada ya kuumia katika mchezo huo wa fainali dhidi ya Ufaransa.

“Nilikuwa katika wakati mgumu sana kwa kuwa nilikuwa na lengo la kuisaidia timu ila baada ya kuumia, nilijikuta ninalia kwa kuwa niliamini ndoto zangu za kuisaidia timu hiyo zimefikia mwisho baada ya kuisi maumivu makali, lakini daktari wangu aliniambia sijaumia sana,” aliongeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles