WATAALAMU WA AFYA KUANZA KUSAJILIWA NA KUPEWA LESENI ILI KUTAMBULIKA

0
868
c80299ae-86e4-4863-8140-4c7a0e123cf7
Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Muhammad Kambi

Wataalamu wa kada mbalimbali zilizopo ndani ya sekta ya afya sasa wataanza kusajiliwa na kupewa leseni ili kutambulika na zitakuwa na masharti maalumu.

Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Muhammad Kambi amesema Serikali tayari imeanza mchakato wa kuipitia upya Sheria ya Madaktari wa Tanganyika ambayo itaongezwa sharti hilo pamoja na kuundwa kwa bodi maalumu ambayo itakuwa ikisimamia maadili ya watumishi hao.

“Sekta ya afya kama zilivyo sekta nyingine nayo imekua, wakati ilipoanzishwa Sheria hii ilikuwa ikiwatambua madaktari na wauguzi pekee lakini sasa hivi kuna taaluma nyingi ndani ya hii fani, hivyo ni vyema kuzitambua kurahisisha ufuatiliaji,” alisema Prof. Kambi

Aliongeza kuwa kila mtumishi atatakiwa kujiendeleza kielimu ili kuongeza ujuzi ili aendane na wakati uliopo kwa sababu mambo yanabadilika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here