27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

TWITTER YAFUNGIA KIMAKOSA AKAUNTI YA MKURUGENZI MTENDAJI WAO

twitter-2
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Twitter, Jack Dorsey

Jumanne hii, majaribio ya kufikia akaunti ya mtandao wa Twitter ya Mkurugenzi mtendaji mkuu wa Kampuni hiyo kubwa, Jack Dorsey haikuzaa matunda baada ya watumiaji wengi kukutana na ujumbe wa makosa uliokuwa unasema kuwa akaunti yake ilikuwa imefungwa.

Ujumbe huo ulisababisha uvumi kuwa akaunti yake inaweza kuwa ilikuwa
imedukuliwa(hacked) au kufungwa moja kwa moja kwa sababu ya idadi kubwa ya malalamiko kutoka kwa watumiaji wengine.

Baada ya kurudi hewani, Dorsey aliweka ujumbe mtandaoni humo akielezea kwamba kusimamishwa kwa akaunti yake ilikuwa ni matokeo ya “makosa ya ndani.” Jibu lililoleta hasira kutoka kwa baadhi ya watu ambao waliuliza jinsi akaunti za watumiaji wengi wa kawaida zinaweza pia kuwa zimesitishwa kimakosa na kampuni hiyo katika siku za nyuma.

Mara baada ya akaunti ya Dorsey kurudishwa, idadi yake ya wafuasi aliokuwa nao ilionyesha kuwa ni 145 tu kutoka takribani watu milioni 3.9 aliokuwa nao hapo awali. Lakini baada ya muda kidogo, takwimu zilibadilika na kupanda hadi kufikia karibu milioni 3.8.

Suala la watumiaji gani ambao Twitter inaweza kusitisha akaunti zao limekuwa suala gumu sana.  Kampuni imekuwa ikijitahidi kupata uwiano mzuri kati ya kuruhusu uhuru wa kujieleza mtandaoni  na kulinda watumiaji dhidi ya unyanyasaji.

 

Dorsey, ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa mtandao huo wa Twitter aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kwanza wa kampuni hiyo kabla ya kuondolewa nje ya kampuni mwaka 2008. Baadaye akarejea katika kampuni na kurudi tena kwenye cheo chake mwaka jana.

 

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles