27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 4, 2023

Contact us: [email protected]

Serikali kujenga vyuo 65 vya Veta nchi nzima

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Katika kuhakikisha wananchi wanainuka kiuchumi kwa kujiajiri na kuajiriwa Serikali imeweka mkakati wakujenga Vyuo vya Elimu na Mafunzo Stadi (VETA) 65 nchi nzima.

Akizungumza leo Julai 12, jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari kwenye maonesho ya 47 ya Biashara Kimataifa Sabasaba baada ya kutembelea banda la Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA), Meneja Uhusiano, Sita Peter amesema lengo la Serikali kuhakikisha inakabiliana na changamoto ya uhitaji wa elimu na mafunzo stadi kwa wananchi kwa kujenga vyuo hivyo.

Aidha, amewataka Watanzania kujitokeza katika maonesho hayo ili kupata elimu inayotolewa na VETA sambamba na kujiunga na chuo hicho.

“Vyuo vya VETA vipo nchi nzima vinafundisha fani mbalimbali vinatoa elimu za ujuzi zote watu waweze kujiajiri wenyewe na kuajiriwa na kupta mahitaji yao muhimu na kuchangia pato la Taifa,” amesema Peter.

Nao baadhi ya Wahitimu kushiriki katika maonesho hayo wamesema wamepata mafunzo ambayo yamekuwa na faida Kwao Kwani wameweza kujiajiri na wengine wameajiriwa katika sekta mbalimbali ikiwemo ya urembo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles