26.8 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

GGML yaipa tano Wizara ya Madini kwa kutoa elimu

*GGML wapongeza Mkaa mbadala wa STAMICO

*GGML kinara uchangiaji huduma kwa jamii

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wizara ya Madini imepongezwa na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kutoa elimu kwa wananchi na wadau wanaotembelea banda la Wizara, taasisi zake na wadau wa Sekta ya Madini.

Pongezi hizo zimetolewa Julai 11, 2023 na Mwanasheria Mkuu wa kampuni ya GGML, David Nzaligo alipotembelea banda la Wizara ya Madini (MADINI PAVILION) katika Maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es salaam.

Akizungumza mara baada ya kutembelea banda la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Nzaligo ameipongeza kampuni hiyo kwa kuleta Mkaa Mbadala wa Rafiki Briquettes ambao utasaidia kudhibiti uharibifu wa mazingira hapa nchini.

Akiwa katika banda la kampuni ya GGML ambalo lipo pia ndani ya banda la madini, Nzaligo amewapongeza wafanyakazi wa GGML na kampuni zingine ndani ya banda hilo kwa kuonyesha weledi mkubwa katika kutoa elimu ya shughuli wanazozifanya ikiwemo uchimbaji madini na mnyororo wake.

“Nafahamu GGML wapo vizuri kwenye miradi mingi ya kijamii pamoja na uwezeshaji wananchi kiuchumi. Nafurahi kwamba mafanikio hayo wanayaelezea vizuri kwa kila mwananchi anayetembelea banda la GGML,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles