29.2 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali imevunja ahadi yake kuhusu mitaala ya somo la dini ya kiislamu-IEP

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

JUMUIYA na Taasisi za Kiislamu Tanzania imeilalamikia Serikali kwa kuvunja ahadi yake ya kuwapa umiliki wa mitaala ya somo la elimu ya dini ya kiislamu.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Septemba 27, 2023 jijini Dar es Salaam na Amir wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania(IEP), Sheikh Mussa Kundecha, akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Jopo la Wataalamu wa Kiislamu, linaloundwa na jumuiya hiyo.

Amesema katika vikao tofauti tofauti ambavyo wameketi na uongozi wa Wizara ya Elimu, akiwemo Waziri wa Elimu, Prof. Adolph Mkenda, kwa ajili ya kuandaa na kuratibu ufundishaji wa dini ya Kiislamu na lugha ya Kiarabu, Serikali iliahidi kuacha umiliki wa somo hilo kwa waislamu, lakini mwisho imeshindwa kutekeleza ahadi hiyo.

“Kinachotutia wasiwasi ni kwamba, katika kikao cha tarehe 12 Agosti 2023, Prof. Mkenda aliomba radhi na kukiri suala hili la umiliki wa mtaala libaki kwa waislamu wenyewe kwamba michakato yote kwenye hili Taasisi ya Elimu nchini(TET) wasiingilie.

“Wakati vikao na michakato yote ikiendelea, kuna mambo yanatatiza bado, hadi sasa ukitembelea tovuti ya TET kwenye kiunga cha mitaala, mihutasari na moduli, ipo mihutasari ya masomo 15 ya dini haijawekwa sababu TET haina haki miliki,”amesema Sheikh Kundecha.

Amesema jambo la kushangaza katika mihutasari ya elimu ya sekondari upo wa somo la elimu ya dini ya kiislamu ambayo imeeleza haki miliki yote ni ya serikali hadi kudurufu ni kosa kisheria bila kupata idhini ya maandishi.

“Kupitia mkutano huu tunaishauri Serikali kuepuka hujuma na uvunjifu wa katiba unaofanywa na baadhi ya watendaji wachache wanaotaka kutumia vibaya nafasi zao,” amesema Sheikh Kundecha.

Akijibu kauli hiyo, Wizara ya Elimu, imekanusha madai hayo huku ikieleza kuwa haijachukua haki miliki ya mitaala hiyo kama ilivyoelezwa na viongozi hao na kwamba jumuhiya hiyo ilitafsiri vibaya na kwamba itatoa ufafanuzi juu ya jambo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles