25.1 C
Dar es Salaam
Monday, May 20, 2024

Contact us: [email protected]

Sekta binafsi kwenye elimu yaokoa fedha za kigeni na kukuza uchumi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wawekezaji binafsi kwenye sekta ya elimu hapa nchini wameokoa fedha nyingi za kigeni baada ya uwekezaji mkubwa kufanywa kwenye eneo hilo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shule za Tusiime zilizoko Tabata-Sanene, Ilala, jijini Dar es Salaam, Dk. Albert Katagira amesema kuwa miaka ya nyuma wazazi wengi walikuwa wakiwapeleka watoto wao nje ya nchi hasa Kenya na Uganda kupata elimu ya msingi na sekondari.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shule za Tusiime zilizoko Tabata-Sanene, Ilala, jijini Dar es Salaam, Dk. Albert Katagira.

“Kabla ya uwekezaji huu tuliofanya, wazazi wengi walikuwa wakisomesha watoto wao nje ya nchi na hivyo fedha nyingi za kigeni kutumika jambo ambalo halikuwa sawa kiuchumi,” amesema Dk. Katigira.

Dk. Katagira pia alisema kuwa sekta binafsi kwenye elimu inaisaidia serikali kupunguza matumizi kwenye bajeti yake kwa upande wa elimu.

“Serikali inasomesha vijana kwenye shule zake tena kwa kutenga fedha kwenye bajeti kila mwaka, kwetu sisi kusomesha vijana tunaisaidia serikali kupunguza matumizi kwenye bajeti yake,” amesema Dk. Katagira.

Sekta binafsi kwa upande wa elimu inasaidia pia kutengeneza ajira kwa maana ya kuajiri waalimu, madereva na watumishi wengine.

“Pia tunatengeneza ajira ambazo si za moja kwa moja kwa maana kwamba watu wanafungua biashara zao kwenye maeneo yanayozunguka shule zetu, utaona kuna maduka mengi, wengine wanafungua mighahawa na stationery,” amesema.

Pia amesema wamekuwa wakiwekeza fedha nyingi kwenye mafunzo yamuda mrefu na mfupi kwa waalimu wao ili waendane na wakati na kutoa elimu bora.

“Huku tunatoa elimu bora kwasababu tumewekeza ndiyo maana uelewa na ufaulu wa vijana wetu unakuwa mkubwa,” amesema.

Naye, Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Tusiime Dk. Laurent Gama ambaye pia ni Mtendaji wa TAPIE Chama cha Wawekezaji binafsi kwenye Elimu nchini anasema uwekezaji wa sekta hiyo ndiyo unaoleta matokeo chanya kwenye mitihani ya mbalimbali ya kitaifa.

Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Tusiime, Dk. Laurent Gama.

Alisema ushirikishwaji ya sekta hiyo kwenye masuala mbalimbali yahusuyo elimu ni muhimu kwani sekta hiyo inatoa mchango kwa watanzania wengi.

Tunapenda kushirikishwa kwenye miradi mbali ihusuyo sekta ya elimu kwani wawekezaji binafsi wanamchango mkubwa kwenye maendeleo ya elimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles