26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Sarah ajivunia kuwaremba wasanii

SARA-MAPUNDA-2-204x300NA GEORGE KAYALA

MREMBO aliyebahatika kukubalika kwa wasanii wa filamu za Kibongo, Sarah Mapunda, amesema kuwa ana kila sababu ya kujivunia kazi ya kuwaremba waigizaji hao kwa kuwafanyia ‘makeup’ ili wawe na mwonekano
mzuri.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Sarah alisema kuwa karibu waigizaji wote wa filamu nchini wamekuwa wakitegemea huduma yake ya make-up na kwa kiasi kikubwa imemfanya aendeshe maisha yake bila kutetereka, hiyo imetokana na wahusika kumkubali.

“Najivunia kufanya kazi ya make-up kwa wasanii wa filamu, kwani huwa wanapendeza wanapoonekana kwenye
filamu zao, hivyo wananikubali kutokana na kuona tofauti na huduma za warembaji wengine,” alisema
Sarah.

Aliwataja baadhi ya wasanii ambao amekuwa akiwaremba wanapoanza kuigiza ambao ni Vicent Kigosi ‘Ray’, Riyama
Ally, Halima Yahya ‘Davina’, Richie Mtambalike, Jacob Steven ‘JB’, Wema Sepetu, Irene uwoya, Aunt Ezekiel na
wengine wengi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles