Bw Hollande alisema hatua hiyo ya Bw Trump si ya busara.
“Ulaya haihitaji ushauri kutoka nje, kuambiwa inafaa kufanya nini,” Hollande alisema.
Katika hili, Trump alisema Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alifanya “kosa kubwa” kwa kuwaruhusu wahamiaji kuingia nchini mwake kwa wingi.
Merkel kwa upande wake, akijibu tamko hilo la Trump, alisema bara Ulaya linafaa kuachwa lijifanyie maamuzi.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry pia alishutumu tamko hilo la Bw Trump.
“Nilifikiri, kusema kweli, kwamba haikufaa kwa rais mteule wa Marekani kuingilia siasa za mataifa mengine kwa njia ya moja kwa moja,” Bw Kerry aliambia CNN.
“Atahitajika kuzungumzia hilo. Kuanzia Ijumaa (siku ya kuapishwa kwa Trump kuwa rais) ambapo atakuwa anawajibikia uhusiano huo.”