24.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 17, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia aalikwa Vatcan na Papa

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Francis amemwalika Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, Vatican Februari 11 hadi 12,2024.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Januari Makamba alipozungumza na Waandishi wa habari mapema leo Januari 21, jijini Dar es Salaam.

Ameeleza kuwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan akiwa Vatican, atakuwa na mazungumzo na Baba Mtakatifu Papa Francis pamoja na Katibu wa Vatican, Pietro Parolin. Uhusiano kati ya Tanzania na Vatican ulianza miaka ya 1960 wakati ambapo Vatican ilianzisha Ubalozi wake hapa nchini.

“Tangu wakati huo Vatican kupitia Kanisa Katoliki imekuwa mstari wa mbele katika kujishughulisha na masuala ya kiroho, amani, elimu na program za afya. Kwenye ziara hiyo Mhe. Rais Samia ataongozana na wawakilishi watano wa waumini wa Kanisa Katoliki Tanzania kutoka kwenye jumuiya mbalimbali za kanisa hilo.

“Vatican kupitia Kanisa Katoliki limechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya sekta ya elimu kabla na baada ya uhuru wa Tanzania Bara kwa kutoa elimu kwa Watanzania wa dini zote. Kupitia shule na vyuo mbalimbali Kanisa kwa kushirikiana na Serikali limechangia kwa kiasi kikubwa kuzalisha viongozi na wataalam mahiri kwenye maeneo mbalimbali,” ameeleza Makamba.

Katika ziara hiyo Tanzania inaangalia fursa za kuanzisha maeneo mapya ya ushirikiano yatakayotoa msukumo mkubwa zaidi kwenye kuimarisha na kukuza amani na usalama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles